Skip to main content
TUMESIKITISHWA SANA NA UKIMYA WA SERIKALI ZETU

TUMESIKITISHWA SANA NA UKIMYA WA SERIKALI ZETU

82 signatures 18 to reach 100
S
Someone signed
M
mulokozi signed
N
Njenga G. signed
S
Someone signed
R
Rajan signed
A
Abdallah C. signed
L
Lyn O. signed
N
Naomi B. signed
K
Khalid S. signed
S
Saida O. signed
IS
Started by Issa Shivji 1 year, 1 month ago
  1. Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni

Rais wa Jamhuri ya Uganda



Mheshimiwa William Samoei Arap Ruto

Rais wa Jamhuri ya Kenya



Sisi, wana Afrika Mashariki, tumesikitishwa na kuaibishwa sana na ukimya wa serikali zetu kuhusu mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza. Ni aibu kubwa sana kuona serikali zetu zikishindwa kutoa kauli hata moja kulaani ukatili unaofanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza.



Kwa maksudi kabisa, Israel inawanyima chakula na hata maji ya kunywa watu wa Gaza, wakiwemo watoto na mama wajawazito. Unyama na ukatili wa kiwango hikii haujatokea duniani kwa karibu karne mbili



Lengo la Israel ni kuua wakazi wote wa Gaza, au kuwahamisha kwa mabavu ili walowezi wa kizayuni waimiliki Gaza. Kwa zaidi ya miaka 75 lengo la Israel limekuwa kupanua mipaka yake ili kumeza nchi nzima ya Palestina pamoja na Gaza na West Bank.



Syio tu kwamba serikali zetu zimeshindwa kulaani haya matendo ya Israel, lakini zinazuia wananchi wake hata kuaandamana, au kwa njia nyingine yoyote, kuonyesha mshikamano wao na binadamu wenzao wa Gaza.



Licha ya kuchelewa sana, tunawasihi na kwa matumaini kuwa, serikali zote tatu zitazinduka na kuchukua msimamo ambao serikali yoyote inayojiheshimu na inayojaali ubinadamu inastahili kuchukua.




51 Comments

I
ISSA SONGOK
1 year ago Featured

Vile vile mashirika za kiislamu kama SUPKEM ya Kenya na BAKWATA ya Tanzania wangepanga maandamano makubwa nchini, tutazuiliwa na Kupigwa lakini kujitolea ndio laugha ambayo serikali zetu zinaelewa.

L
Leonard Mselle
1 year ago Featured

Ahadi za Mwana-TANU 1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja. 2. Nitajitolea nfsi yangu kuondoa nujinga, maradhi na dhuluma. Watanzania mliokomboa kusini mko wapi?

M
Mahir Meghji
1 year ago Featured

What is happening in Gaza is unbearable. Children are short as a target practice, starved to death. This is not just tragedy, it’s a crime against humanity- Genocide. I urge our Government to take stand and publicly condemn Israel’s actions. Our Government silence is not neutral. It is complicit. If you stay silent now, history will not.

H
Hermes Damian
1 year ago Featured

Hakika, tunaugua kwa ukimya wa salerikali zetu. Kama ziko kwenye shinikizo la kutokukosoa ukatili huu. Kwa ukimya wenu mmetufanya sote tuwe Kama tunaunga mkono undamaged huu. Najiuliza, je, serikali hizi zingekuwa madarakani wakati nchi za Afrika kikipambana kukomboa nchi nyingine kama Afrika kusini wangefanya jambo kweli ama wangekaa kungoja watesi waamue hatima ya wenzetu?

C
Capt Ibrahim Mbiu Bendera
1 year ago Featured

Tolerating Israel is supporting what they & their friend USA are doing; killing children & their mothers with HUNGER! Conducting apartheid policy by killing Palestinians, destroying their country and denying them their free Palestine State. WE, EAC Sates should close our embassies in Israel and cut off diplomatic ties with them.

S
Sabatho Nyamsenda
1 year ago Featured

Tunazitaka Serikali za Afrika Mashariki kusimama katika upande sahihi wa historia. Zilaani na kuchukua hatua kali dhidi ya uzayuni, ambao kiuhalisia ni ukaburu ulio na lengo la kuwateketeza Wapalestina na kutwaa ardhi yao. From the river to the sea, Palestine shall be free.

A
Anonymous
7 months ago

Na mauaji ya kwetu pia

M
mulokozi
1 year ago

Kweli inabidi Waafrika tufanye jambo kuhusiana na mauaji haya!

Help this petition grow

Share it with friends to help reach 100 signatures.

Your share link

Share directly