Mahamudu Rashidi Hussein 0

Sema HAPANA kwa mapendekezo ya mabadiliko ya udahili katika kada ya Uuguzi.

321 people have signed this petition. Add your name now!
Mahamudu Rashidi Hussein 0 Comments
321 people have signed. Add your voice!
33%
Maxine K. signed just now
Adam B. signed just now

Kama mtakumbuka katika Maazimisho ya siku ya wauguzi ambayo kitaifa yalifanyika Katavi huku katika mkoa wa Dar es salaam yakifanyika Hispitali ya taiga ya Muhumbili.
Katika Maazimisho hayo katika hispitali ya Taifa Msajili wa wakunga na wauguzi alidai siku ya Tarehe 12/05/2019 walikaa kikao na wadau mbali mbali ili kuweza kupunguza alama za udahili katika vyuo mbali mbali kwa kada ya uuguzi.
Sababu kuu aliyoitoa ni kuwa Vyuo vya private vinakosa udahili wa wanafunzi na pia alidai kuna uhaba wa wauguzi.
Madhara ya maamuzi haya.
Maamuzi haya yanairudisha fani ya uuguzi hatua 10 nyuma kwani kama mtakumbuka Uuguzi ulitambulika kuwa ni fani ya waliofeli. Watu walipigana na taswira hiyo imekua ikiondoka taratibu.
Pia hili litawapa wauguzi tabu katika ngazi mbali mbali za maamuzi kwani wataonekana kuwa na kiwango cha chini cha elimu na ufaulu.
Nini cha kufanya.
Nimeamua kuandaa Petition hii ili kuwapa nafasi wauguzi wote wanafunzi na ambao sio wanafunzi kupinga swala hili.
Hivyo sambaza ujumbe huu kwa Wauguzi wote.
Tunahitaji saini zaidi ya 20,000.

Share for Success

Comment

321

Signatures