Skip to main content

Sema HAPANA kwa mapendekezo ya mabadiliko ya udahili katika kada ya Uuguzi.

279 Comments

A
Anonymous
7 years ago

Hatupo tayari heshima ya uuguzi kushushwa hadhi kiasi hicho

A
Agustino Tsoray
7 years ago Featured

Napinga kigezo cha kushusha viwango vya udhahili Cha kufanya vyuo vya watu binafsi wapunguza gharama kwa mana ya ada waridhike na kidogo tunajua ni biashara yao Tuwaandae vizuri wachache tunaowapata mwisho tuwe na professional enye heshima kwetu na kwa dunia nzima

M
Mary
7 years ago

Napinga hili suala la kushusha viwango kwa udahili wa wanafunzi wa nursing , tunaelekea wap ,???WHY THIS NI SAWA NA KUMRUDISHA MTOTO ANAETEMBEA KUANZA KUTAMBAA UPYA , jaman tufikir kabla ya kutenda, , , ,

A
Andrew
7 years ago

Maamzi ya kushusha grade kwa kada ya nursing ni kuishushia heshima ni jambo lisilo kubalika.

I
irene
7 years ago

sihafiki uuguzi ni kazi inayopaswa kuheshimiwa mno na inahitajika watu wenye ufaulu Mzuri ukizingatia Tunakaa na wagonjwa masaa mengi kutatua matatizo yao.

A
Anonymous
7 years ago

They should employ those nurses who are note employed.

M
MUSA LAITON MKWAMA
7 years ago

Haya ni maoni yng kuhusu zoezi la kutaka kubadili vigezo vya udahili kwa wanafunzi wa stashahada. =vyuo vya binafsi kukosa wanafunzi wauguzi hakusababishwi na vigezo vya udahili bali ni gharama kubwa za ada ya masomo ambazo wazazi wengi hushindwa kumudu na katika hili hata serikali yetu pendwa imekuwa ikipiga kelele kwa taasisi binafsi kuweza kupunguza ada hizo ili wazazi wengi waweze kumudu kuwapeleka watoto wao. =upungufu wa wauguzi kuanzia kwenye ngazi ya zahanati hausababishwi na kutokuwepo kwa wauguzi wahitimu au wauguzi wachache hapana, wauguzi wapo wa kutosha mitaani ambao hawajafanikiwa kupata ajira, hvy upungufu wa wauguzi mahospitalini hautokani na vigezo vya udahili ambavyo kwangu binafsi ni bora kwa hatma nzuri ya taaluma yetu. = uuguzi upo tofauti kabisa na kada kama CO,MED LAB,PHAMACY. Muuguzi mwenye ngazi ya stashahada huyu anauwezo wa kufanya kazi kimataifa tofauti kbs na kada zingine katika ngazi ya stashahada hvy ni lazma tuwe na vigezo visivyo na shaka ndani ktk udahili ili tuweze kuzalisha wauguzi ambao wanauwezo wa kufanya kazi kimataifa pasipo shaka. = sisi kama wauguzi hatupaswi kuwa watu wa kuweka vigezo virahisi ili tuweze kufurahi kuzalisha wauguzi wengi hovyo wenye vigezo vya hovyo ni lazima tuimarishe kada yetu hii ikiwa ni pamoja, lakini pia tuondokane na fikra kwamba uhaba wa wauguzi ni kutokana na vigezo vya udahili ingali tunao wengi mitaani wasio na ajira. NOTE SIUNGI MKONO MABADILIKO HAYO KWANI C SURUHUSHO LA KUWA NA WAUGUZI WENGI.

A
Anonymous
7 years ago

Sikubaliani Na tamko la kushusha vigezo vya kudahili wauguzi.

M
MASSAY
7 years ago

This is very great hazards to nursing plz let us be one voice to against this kind of nursing suicide, nursing cyo dampo Binafsi naipinga wazo LA kushusha grade, Tujue tunadili Na binadamu

G
Golden Mwakibo
7 years ago

Lowering the entry qualifications amid our eyes is steping on efforts made by nurses themselves over the past 17 years of reformation of Nursing in Tanzania. We want to see the new generation of nurses who are cognitivelly intelligent, who can stand on their own feet amid other professions. Lowering their entry qualification is against this viewpoint.

J
John Reuben
7 years ago

Against it

C
Charles
7 years ago

TNMC/TANNA tafadhali Msitafte kuturudisha tulikotoka... Msituletee vilaza walio na marks za kudidimia.. Hawana akili kubwa.. Hatutaki...

J
Joshua
7 years ago

Tusishushe hadhi ya taaluma ya uuguzi kwa kushusha vigezo vya kujiunga na taaluma hii.

J
Jactan Gatuku
7 years ago

Uuguzi ni taaluma inayohitaji weledi wa hali ya juu. Kupunguza vigezo vya udahili kutataoa nafasi ya kuufanya uuguzi kuwa kimbilio la watu walioshindwa kufaulu. Hili litapelekea kazi kiuguzi kufanyika kwa ufanisi na weledi mdogo kwa sababu zitakuwa zinafanywa na watu ambao waliamua kuwa wauguzi kwa sababu walishindwa kupata alama za kuwawezesha kusoma fani nyingine. Pia inashusha hadhi ya taaluma ya uuguzi na wauguzi. Ule msemo wa 'hata nursing huwezi kwenda' ulikuwa umeanza kupotea utaanza kurudi tena. Tutarajie watu wenye viwango vizuri vya ufaulu na weledi watakuwa wakiwaza namna za kuukimbia uuguzi na kuwaachia wale ambao hawana vigezo. Uuguzi utarudi kuwa kazi ya 'wajinga' na tutarajie huduma zitakazotolewa zitakuwa za kijinga pia. Ni aibu kubwa kwa watu wote waliokaa na kuamua kupitisha uamzi huo wa 'hovyo' wa kushusha vigezo vya kujiunga na uuguzi. Wanapaswa wajitafakari, wajipime kama bado wana sifa za kuendelea kuaminiwa katika nafasi walizoaniwa na kupewa.

E
Erai Erasto
7 years ago

Mimi sikubaliani na hayo malengo ya msajili. Hivyo vyuo vyenye upungufu was wanafunzi warudie kuangalia ada zao. Ili wapate wanafunzi wengi Pili Naomba aangalie faida ya kuwa na wanafunzi wengi alafu vifo vikaongezeka. Asirudishe nyumba ambako tunakukimbia, tunahitaji heshima ya taaluma na sio kuwa taaluma ya waliofeli. Nawasilisha

T
Theresia
7 years ago

Wauguzi badala ya kwenda Mbele sisi tunarudi nyuma...kwa hali hii lazima tutaendelea kuzalaulika tu..Upungufu wa wauguzi siyo issue ya kupunguza Alana katika udahili..kuna amnesia kibao mtaani wanahangaika kutafuta Kazi toka 2015 ,Serikali inaajiri kidogo kidogo.......Viongozi wetu shaurini Serikali kuajiri zaidi badala ya kupunguza igezo vya udahili....Tatizo la vyuo binafsi kukosa wanafunzi wengi siyo issue ya Vigezo wengi tunashindwa kulipia ada zenu

L
Lightness harold
7 years ago

Napinga kabisa hii n kurudisha nyuma taaluma, tumepiga atua bafo tena mwataka turud tuliko toka...

M
Mwajuma
7 years ago

I say no to it

S
Shabani Selemani
7 years ago

Kweli kabisa hakuna sababu yenye mashiko ya kushusha vigezo vya udahili kwa wauguzi. Hivi najiuliza watu wanaotoa maamuzi kama haya ambayo kwa akili ya kawaida tu unaona haiingii akilini hivi walisomea wapi, namashaka na elimu zao

R
Ruda Paul
7 years ago

Ili kada yetu iheshimiwe lazima tuwe na watalaam waliobobea na wenye elimu kubwa. Kushusha Gred Ni sawa na kuendelea kuirudisha kada yetu nyuma.