TUMESIKITISHWA SANA NA UKIMYA WA SERIKALI ZETU
- Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni
Rais wa Jamhuri ya Uganda
Mheshimiwa William Samoei Arap Ruto
Rais wa Jamhuri ya Kenya
Sisi, wana Afrika Mashariki, tumesikitishwa na kuaibishwa sana na ukimya wa serikali zetu kuhusu mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza. Ni aibu kubwa sana kuona serikali zetu zikishindwa kutoa kauli hata moja kulaani ukatili unaofanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza.
Kwa maksudi kabisa, Israel inawanyima chakula na hata maji ya kunywa watu wa Gaza, wakiwemo watoto na mama wajawazito. Unyama na ukatili wa kiwango hikii haujatokea duniani kwa karibu karne mbili
Lengo la Israel ni kuua wakazi wote wa Gaza, au kuwahamisha kwa mabavu ili walowezi wa kizayuni waimiliki Gaza. Kwa zaidi ya miaka 75 lengo la Israel limekuwa kupanua mipaka yake ili kumeza nchi nzima ya Palestina pamoja na Gaza na West Bank.
Syio tu kwamba serikali zetu zimeshindwa kulaani haya matendo ya Israel, lakini zinazuia wananchi wake hata kuaandamana, au kwa njia nyingine yoyote, kuonyesha mshikamano wao na binadamu wenzao wa Gaza.
Licha ya kuchelewa sana, tunawasihi na kwa matumaini kuwa, serikali zote tatu zitazinduka na kuchukua msimamo ambao serikali yoyote inayojiheshimu na inayojaali ubinadamu inastahili kuchukua.
Enter your details on the next page
Comment
See More 0