Skip to main content

Sema HAPANA kwa mapendekezo ya mabadiliko ya udahili katika kada ya Uuguzi.

25 Comments

J
Joseph C Nsongo
7 years ago

Nakataa maamuzi ya TNMC kuhusu kushusha vigezo vya udahili wa wanafunzi katika nursing school ..vigezo vibaki Kama ilivyo kwa sasa

G
George Mbalilwa
7 years ago

Kushusha marks za udaili ili kupata manesi wengi ni kuidumaza idala kumbuka kuna vijana wengi walisoma diproma wakiwa na vigezo vyote TNMC kashindwa kuwapatia lesen baada ya kutofanya vzr mitihan yao ya diproma

L
Lujani Hoho
7 years ago

Kitendo cha kushusha Admission criteria ya student nurses kujiunga na chuo siyo njia ya kukidhi mahitaji wa wauguzi nchini Bali ni mikakati aidha ya makusudi au bahati mbaya ya kuiangamiza taaluma ya uuguzi. Njia nzuri ni kuboresha mifumo kwanza ya destination ya muuguzi baada ya kuhitimu mafunzo ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi, kuwalinda wauguzi wakiwa katika vituo vyao vya kazi (jambo hili linaathili sana maamuzi ya watanzania kuendelea au kutokuendelea kupeleka watoto wao kusomea uuguzi, wanasiasa wamewajengea wananchi tabia ya kuwaona wauguzi kama adui zao badala ya rafiki zao na kimbilio lao wakati wa ugonjwa na udhaifu kiafya. Tabia hizi zina wafanya wananchi kuona kwamba muuguzi hayuko salama. Na kama tunavyojua, hakuna mtu angependa kufuata njia ambayo anaona waliotangulia kuipita wameteswa na kuuawa. Kwa hiyo hapa so swala la kushusha pass mark Bali ni swala la kutengeneza mfumo mzuri na salama kwa muuguzi akiwa shule na atakapokuwa katika kituo cha kazi na uraiani. Tuondoe kwanza hofu kwa wananchi juu ya tishio la kiusalama wa muuguzi, Nina imani kubwa tunaweza kuwavuta watanzania wengi kujiunga na mafunzo katika taaluma ya uuguzi. Na jambo la mwisho japo si kwa umuhimu ni swala la masilahi ya muuguzi: 1. kupewa mishahara inayoendana na majukumu makubwa na magumu aliyonayo muuguzi 2. Kupewa motisha mbalimbali za kimazingira na kiutendaji anapokuwa akitekeleza majukumu yake. Hii ni pamoja na zamu za usiku, kufanya kazi katika mazingira yenye hatari ya kuambukizwa magonwa yakiwemo yasiyo na tiba kama vile HIV na Hepatitis, kupata ulemavu wa muda au wakudumu akiwa anatekeleza majukumu yake ya kuokoa uhai wa wagonjwa na kutoa tumaini kwa familia zao nk. 3. Kupewa utambuzi maalumu mbali mbali pale muuguzi anapofanya kazi zake kwa kiwango na ubora wa hali ya juu. NINQOMBA BARAZA NA WADAU KWA PAMOJA TUACHE KABISA KUSHUSHA VIGEZO VYA KUJIUNGA KATIKA MAFUNZO YA UUGUZI.

A
Anonymous
7 years ago

Hii haikubaliki kabisa

J
Joshua Deus
7 years ago

Tusishushe viwango