Skip to main content

Status: Closed — this petition is no longer accepting signatures.

Sema HAPANA kwa mapendekezo ya mabadiliko ya udahili katika kada ya Uuguzi.

Sema HAPANA kwa mapendekezo ya mabadiliko ya udahili katika kada ya Uuguzi.

Closed — 28 supporters Verified

Final supporters

S
Someone
T
Tumaini S.
N
Neema Y.
S
Someone
R
Renfrida K.
S
Someone
A
Amina S.
M
moses m.
S
Someone
M
Mpoki N.
+18 more
MR
Started by Mahamudu Rashidi Hussein 7 years, 4 months ago

Kama mtakumbuka katika Maazimisho ya siku ya wauguzi ambayo kitaifa yalifanyika Katavi huku katika mkoa wa Dar es salaam yakifanyika Hospitali ya taifa ya Muhumbili.

Katika Maazimisho hayo katika hospitali ya Taifa Msajili wa wakunga na wauguzi(TNMC) alidai siku ya Tarehe 12/05/2019 walikaa kikao na wadau mbali mbali ili kuweza kupunguza alama za udahili katika vyuo mbali mbali kwa kada ya uuguzi.

Sababu kuu aliyoitoa ni kuwa Vyuo vya private vinakosa udahili wa wanafunzi na pia alidai kuna uhaba wa wauguzi.Hizi si sababu za kutaka kubadili alama za udahili, Msajili na wadau hao warudi tena katika meza watafute njia sahihi ya kutatua changamoto hii.


Madhara ya maamuzi haya.

Maamuzi haya yanairudisha fani ya uuguzi hatua 10 nyuma kwani kama mtakumbuka Uuguzi ulitambulika kuwa ni fani ya waliofeli. Watu walipigana na taswira hiyo imekua ikiondoka taratibu.

Pia hili litawapa wauguzi tabu katika ngazi mbali mbali za maamuzi kwani wataonekana kuwa na kiwango cha chini cha elimu na ufaulu hivyo maamuzi yao hayatotiliwa mkazo.


Nini cha kufanya.

Nimeamua kuandaa Petition hii ili kuwapa nafasi wauguzi wote wanafunzi na ambao sio wanafunzi kupinga swala hili.

Hivyo sambaza ujumbe huu kwa Wauguzi wote.

Tunahitaji saini zaidi ya 20,000.

Updates

May 14, 2019

I am truly humbled by the passion I see in the comments here. The stories you are sharing about the reality of our profession reveal that this is your movement, not mine.

25 Comments

N
Neema Yasin
7 years ago Featured

Shortage na kukosa udahili wa vyuo vya private haitoshi kuwa sababu ya kushusha vigezo, nursing haiangalii practice peke yake ambayo hata medical attendant anaweza kufanya, it is about knowledge, critical thinking and decision making ili unaporud kwenye practice lazima tutoe rationale. So for failures nahisi the best way to help them through is to give them second chance to resit the o'level exam and get what is needed to be admitted for the course. Asiyekubali kurudi shule Basi ujue haipendi nursing alikuja tuu kwa sababu kafeli na huko private anajua atapitapita tuu halafu ataelewa akifika kazini Sasa tujiulize mpaka akija kuelewa atakua keshaumiza wangapi, we have a lot of these people's at work! Vzur tungeanza na hawa.

I
Irene moshi
7 years ago Featured

Kupunguza viwango vya udahili sio suluhisho la ukosefu wa wanafunz vyuoni. Vyuo binafsi viangalie ada wanazopanga wananchi wa hali ya chini wanashindwa kumudu gharama za Masomo. Kushusha grade ni sawa na kuidhalilisha taaluma na sidhan kama watakua wapo radhi kwenda kusomea taaluma inayodharaulika

A
Anonymous
7 years ago Featured

Mimi siungi mkono ushusjwaji wa vigezo vya kujiunga na taaluma hii ya uuguzi, kwanza kabisa kwasababu najua na ninaifanyia kazi hii taaluma na ninaona ni jinsi gani inahitaji watu makini na wenye ujuzi na elimu ya kutosha. Lakini pia tusirudi nyuma pale ambapo ilionekana ni taaluma ya watu waliofeli kujiunga na taaluma zingine. Hii ni sehemu srnsitive inahitaji maboresho mengi lakini sio ya kupunguza vigezo bali kufanya tafiti na kufahamu kua kama kuna uhaba wa wafanyakazi na wanafunzi unatokana na nini?

A
Anonymous
7 years ago

Nursing shida siyo uhaba wa wauguzi shida ni uhaba wa ajira. Na watahiniwa wengi wapo mtaani pasi na ajira.

T
Tumaini Soine Mollel
7 years ago

Hapana

R
Renfrida Kalinga
7 years ago

I strong disagree the situation of changing the criteria for registering diploma and certificate of Nursing

A
Anonymous
7 years ago

What is going to happen here is like making nursing as somewhere people can go when they have no where else, which will make nursing a disrespectfull professional! Please let we stand for our proffesional!

A
Amina Said
7 years ago

Napinga mapendekezo