ALI PANDU 0

SAY NO TO TBS ON THIS DUBIOUS DEAL

3630 people have signed this petition. Add your name now!
ALI PANDU 0 Comments
3630 people have signed. Add your voice!
73%
Maxine K. signed just now
Adam B. signed just now

Sisi watanzania tuishio Uingereza tunapinga utaratibu mpya uliotungwa na TBS kwamba katika kuhakikisha magari yanayasafirishwa kwenda Tanzania yakaguliwe ubora wa kuwepo barabarani kwa kufanyiwa ukaguzi na kampuni moja tu. Kampuni ya WTM UTILITY SERVICES haina historia wala uzoefu wowote wa kukagua magari iweje wapewe mkataba huu Tunataka kufahamishwa vigezo vilivyotumika kuwapatia WTM UTILITY SERVICES mkataba huu. Mfumo wa kukagua magari na viwango vya magari ya Uingereza ni vya hali ya juu, Kwa kawaida gari zote zilizopo nchini Uingereza zinatakiwa ziwe na ubora wa kiwango fulani ili kuendeshwa kihalali, ubora huu wengi unajulikana kama MOT. Mafundi walioidhinishwa kufanya hiyo MOT hapa Uingereza wapo zaidi ya laki moja nchi nzima. Kampuni ya WTM Utility Services inachokifanya sio zaidi ya hiyo MOT. MOT ya halali Uingereza inalipiwa paundi 45 tu. Hawa jamaa wa WTM Utility Services wanatoza paundi mia moja kwa kila gari! Huu ni utaratibu ambao haukubaliki. Watanzania waishio Ughaibuni wana hamu na dhamira ya kuwekeza Tanzania taratibu kama hizi zinakwamisha na kupunguza dhamira yao hii. Sisi watanzania tuishio Uingereza hatuikubali hatua hii na tunaipinga. TUNASHAURI: 1. Mkataba kati ya Shirika la viwango Tanzania {TBS} na Kampuni changa isiyo na uzoefu ya WTM UTILITY SERVICES ufutwe kwani haukuzingatia vigezo halisi vya ukaguzi wa magari na urahisi uliopo kuhakikisha hilo. 2.Tunakubali Tanzania sio dampo na haiwezekani kabisa kwa nchi yetu kupokea kila takataka za dunia. Hivyo basi tunashauri sheria mpya itungwe kudhibiti hayo na sheria hii iweke wazi ubora unaokubalika. Kama haja ni kudhibiti ubora wa magari yatokayo Uingereza, cheti cha MOT kinakubalika kabisa duniani kote, itangazwe kwamba gari inayopelekwa Tanzania lazima iambatane na cheti cha MOT la sivyo adhabu kali ikiwemo faini na kuteketezwa kwa gari husika itachukuliwa. 3. Kwa vile utaratibu umetangazwa rasmi tarehe 26.05.07 wakati sheria yenyewe imeanza kazi tarehe 14.05.07 tunaitaka mamlaka ya viwango Tanzania kuondoa ya asilimia arobaini ya thamani ya gari ifutwe kwa magari hayo. 4. Tunaitaka jumuiya ya watanzania Uingereza isimamie maslahi yetu watanzania, tumesikitishwa na hatua za dhahiri za Mwenyekiti wa Jumuiya kuonyesha kuwa yupo upande wa kampuni hii. Mwenyekiti Bwana Abu Faraji, kupitia tovuti yake binafsi www.tzuk.com alitangaza kampuni kuanza kazi zake katika hili, Mwenyekiti huyo huyo ametoa tamko baadae kwamba anashangazwa na hisia mbaya walizonazo watanzania na kuwasihi wawe watulivu, huu ni utapeli haukubaliki na tunamtaka mwenyekiti achukue hatua kuonesha dhahiri anawakilisha maslahi ya watanzania na sio rafiki zake wa karibu. 5. Tunawaomba watanzania wanaosafirisha magari yao kwa sasa wagome kufanya uchunguzi huo na pia wagome kulipa faini magari yakifika Tanzania, badala yake tufungue kesi mahakamani Tanzania kuhoji uhalali wa hatua hii. Kama gari la mtanzania halina MOT basi ajitahidi afanye MOT kabla ya kusafirisha KUTOKA KITUO CHOCHOTE CHA MOT HAPA UINGEREZA. Tunawasihi watanzania wakati wa kuoneana haya na kuogopana umekwisha, tafadhali elezea hisia zako kwa kusaini petition hii, huhitaji kutoa jina lako bali kuweka maoni yako tu kutasaidia sana. Tunakushukuru ndugu mtanzania kwa moyo wako wa kizalendo.

Share for Success

Comment

3630

Signatures