
SHIRIKI KUPINGA MAUAJI YA ALBINO TANZANIA


Ndugu, Kwa muda mrefu sasa nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na wimbi la mauaji ya ndugu zetu Albinos.Pamoja na kulaaniwa na wanajamii wengi na hatua mbalimbali ambazo serikali imejaribu kuzichukua,wimbi la mauaji limezidi kuenea.Hivi leo,wenzetu hawana amani tena ndani ya nchi.Maisha yao yanatishiwa kila kukicha. Wimbi hili limezidi kuipaka nchi yetu matope.Kama wanajamii,hatuwezi kukaa kimya.Ni wazi kwamba juhudi za ziada zinahitajika kutoka serikalini ili kukomesha mauaji hayo ambayo msingi wake ni imani potofu kwamba viungo au sehemu mbalimbali za mwili wa albino ni njia mojawapo ya kujipatia utajiri. Ni kwa kuzingatia hilo unaombwa kushiriki katika kupinga,kulaani na kuishinikiza serikali iongeze juhudi za kupambana na janga hili ambalo limeshakuwa la kitaifa.Unachotakiwa ni kutia sahihi.Zikitimia sahihi 100,000,zitapelekwa kwa Waziri mhusika kufikisha ujumbe kwamba juhudi za ziada zinahitajika.Tafadhali shiriki.Asante
Comment