Balozi Daraja Ajiuzulu!
Balozi zetu nyingi zinalalamikiwa kwa kutowajali Watanzania na kutoa huduma duni za kibalozi na ushirikiano kwa Watanzania katika nchi zilizopo. Ubalozi ambao bila ya shaka unaongoza malalamiko hayo ni ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ambapo mkuu wake ni Balozi Andrew M. Daraja. Kwa kuzingatia ukweli kuwa Balozi Daraja ameshindwa vibaya katika mambo kadhaa ambayo yanaanishwa hapa: http://www.mwanakijiji.podomatic.com. Miongoni mwa hayo: a. Kushindwa kutekeleza diplomasia ya Kiuchumi kama ilivyoelekezwa na Wizara ya Mambo ya nje kwa kutumia makabrasha mbalimbali na semina ya mabalozi ya Bagamaoyo. b. Ameshindwa kujenga mahusiano na Watanzania waishio Marekani na hivyo kutowatumia ipasavyo katika kutekeleza diplomasia ya kiuchumi na hivyo kusababisha Watanzania kutokuwa na imani na balozi huyo. c. Ameshindwa kutumia nafasi iliyopo ya uhusiano mzuri kati ya Marekani na Tanzania kunufaisha Tanzania kwa kuvutia watalii wengi zaidi na wawekezaji wengi zaidi na biashara ya Marekani kwa kutumia AGOA, mkataba wa Anga huru. Hivyo basi sisi Watanzania tunatoa mwito wa kumtaka Balozi Daraja ajiuzulu au Rais aamua kumwondoa katika wadhifa huo muhimu ili kutoendelea kupoteza muda mwingi.
Comment