Paul Mongi Kilimanjaro 0

BUNGE LIVE NOW

30 people have signed this petition. Add your name now!
Paul Mongi Kilimanjaro 0 Comments
30 people have signed. Add your voice!
3%
Maxine K. signed just now
Adam B. signed just now

TAMKO:
Sisi, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunatumia haki yetu ya Kikatiba kutoa maoni yetu, kuhusu kitendo kiovu cha Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ifuatavyo:

  1. Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 18-2, inayosema "Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii",
  2. Kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 8(1)-a "wananchi ndio msingi wa MAMLAKA YOTE na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujubu wa Katiba hii",
  3. Na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba hii, "Ibara ya 8(1)-c, Serikali itawajibika kwa wananchi", na "(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii",

Tunatoa tamko lifuatalo:

  1. Serikali imekiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwanyima wananchi haki yao ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali mchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia, juu ya masuala muhimu kwa jamii, HUSUSAN matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Serikali imetoa kisingizio kwamba gharama za matangazo hayo ni Shilingi za Tanzania Bilioni 4 kwa mwaka, lakini imekataa kupokea michango ya gharama hizo kutoka kwa wananchi, bila kutoa sababu za kuridhisha, hata pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari nchini vilipojitolea kubeba gharama hizo moja kwa moja na kutangaza matangazo hayo

Sisi Wananchi, raia wa Tanzania, tumeamua kufanya yafuatayo:

  1. Tutaaacha kununua magazeti yanayochapishwa na vyombo vya habari vinavyosimamiwa na Serikali
  2. Tutaacha kusikiliza vituo vya redio na luninga vinavyoendeshwa na Serikali
  3. Tutafanya hivi kwa kipindi kisichopungua siku 30, baada ya muda usiopungua saa 72, ambazo tunaitaka Serikali iwe imerejesha mfumo wa matangazo ya moja kwa moja kupitia kituo cha luninga cha TBC1, ambacho kinaendeshwa kwa kodi za wananchi, yaani SISI, ambao kwa mujibu wa Katiba "ndio msingi wa MAMLAKA YOTE"!


Serikali yet IMEASI. Imetunyanyasa vya kutosha, imetupuuza vya kutosha, sasa tunasema, hatutanyanyaswa tena na hatutapuuzwa vya kutosha.

HITIMISHO:
Iwapo maendeleo ya kweli yanapaswa kufanyika, ni lazima wananchi wahusishwe! - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Share for Success

Comment

30

Signatures