| # | Name | Comments |
|---|
| 1 | Jumanne Kizinda | |
| 2 | Anonymous | Tanzania kawaida ni nchi ya amani. Inasikitisha kuona ndugu zetu wanaishi katika maisha ya hofu. Serikali inabidi iishugulikie hii case ki undani. Kwanza kuwaadhibu vikali wanaofanya vitendo hivi ili liwe fundisho kwa wengine, hizi societies zinazovanya vitendo hivi zinabidi zielimishwe kwamba utajiri haupatikani kwa njia hii bali kwa kazi ngumu. Waganga wa kienyeji nao inabidi wakamatwe maana ndiyo wanaowapotosha hawa watu wanao ota utajiri wa haraka.
Police wanao shughulikia case hizi wanadai kwamba ni vigumu kuwatia nguvuni wahusika. Kama ni hivyo inabidi serikali ijitahidi kwa hali na mali i waprotect ndugu hawa ndugu zetu walio hatarini either kuweka guard kwenye mikoa hii au kuwa temporary shelter mpaka wakati campagn ya kutokomeza vitendo hivi itakapofanikiwa. PENYE NIA PANA NJIA. |
| 3 | George Mwangosi | Ni lazima hili janga likomeshwe kabisa. |
| 4 | john masela | nalaani vitendo hivi vya kikatili |
| 5 | Jeff Msangi | |
| 6 | Emanuel Gingi | Ma albino ni binadamu kama binadamu wengine na wana haki ya kuishi na kuthaminiwa. Wale wanaoshiriki katika mauaji yao aidha kwa tamaa za utajiri au kwa sababu wanazozijua wao si tu kwamba hawana utu na utashi bali ni watu wa kulaaniwa na kutengwa na jamii ya watu waliostaarabika. |
| 7 | Angelina G. Waniha | Albino ni watu kama sisi, kasoro ya ngozi isiwafanye waonekane si binadamu kama sii. Napinga vikali mauaji ya Abino |
| 8 | Anonymous | Napinga mauaji haya ya albinos, na wanahitaji kupewa haki zao kama watu wengine. |
| 9 | Nicky | This is rediculous. Goven't need to do something about this. |
| 10 | Terry | |
| 11 | Naomi | |
| 12 | Lilian | |
| 13 | Ladslaus Modest | Mauaji ya Binadam awaye yote ni dhambi kwa Mungu na Uharamia mkubwa.
Hii inadhihirisha jinsi gani baadhi ya Watanzania wenzetu wasivyokuwa na IMANI kwa MUNGU Muumba wa Mbingu na nchi ambaye ndiye mtoa rizki kwa kila binadam.
Ni vyema wahusika wote wakamatwe na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria. |
| 14 | hans | kwa kweli inasikitisha sana, mnawafanya jamaa wajisikie kama wapo ugenini! tena kwa kifo! ni utajiri gani huo mnaoutaka kwa kuua wenzenu?
Kuweni na huruma jamani, nao ni binadamu kama wewe, huo utajiri kweli utaula kwa amani wakati unajua umeupata kwa kuua mtu! |
| 15 | Rodney | Mauaji hayo yapigwe vita kabisa. Wanaohusika wakamatwe na kunyongwa. |
| 16 | henry Meleki | Kwa kweli nimesikitishwa sana na mauaji ya hawa watanzania wenzetu. Mawazo yangu ni kwamba serikali na wananch wenyewe tunatakiwa tuwe kitu kimoja katika kukabiliana na hili.
Sifa yetu ndani na nje ya nchi inatiwa doa na wachache wenye imani potofu.
Jeshi la polisi lenyewe haliwezi maliza tatizo tunatakiwa kuwafichua wanaojihusisha na hivi vitendo bila woga. |
| 17 | Anonymous | I condemn the killing of your fellow bro and sisters!
govt please act immediately and bring justice to our society!! |
| 18 | Chris | It's time to wake up and move on. |
| 19 | Pius Pius Mikongoti | Kiukweli hiki ni kitendo cha kulaaniwa na kisichofaa kuungwa mkono na wapenda haki za binadamu.
Serikali inaweza kufanya kwa kuongeza nguvu kwenye hili.
Haki sawa kwa wote. |
| 20 | PAUL CHARLES MUHANGWA | Ndugu,
Kwa muda wa miezi imepita tangu wingi la mauaji ya Albinos limepita na bado linaendelea katika sehemu mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania,Hii ninasababishwa na imani potofu miongoni mwa watu wa hapo Tanzania.
Tatizo hili hasa linasababishwa na Waganga wa Kienyeji ambao hutumia viongo vya Maalbino hao kwa ajili ya dawa zao za kienyeji.Vitendo hivi vinafanyika hasa katika jamii ya Wasukuma yaani Mkoani Mwanza hasahasa Wilayani Sengerema.
Kwa hiyo ninaishauri serikali ichukue hatua kwa wale wote Waganga wakienyeji ambao wanahusika na vitendo hivi vya mauaji ya Albino maana ni binadamu kama wengine hapa Tanzania. |
| 21 | Hidaya Shomvi | nalaani vikali mno vitendo hivi ya kuwaua maalbino kwa imani za kishirikina. |
| 22 | Matty | Nalaani vikali sana hiki kitendo cha baadhi ya watu wenye imani potofu wanao ua na kutoa sehemu nyeti za miili ya Albino.
Jueni ya kwamba binadamu wote ni sawa na sote tumeumbwa na Mungu, jamani inatia uchungu sana kiumbe wa Mungu asiye na hatia anauawa pasipo sababu!
Enyi wauaji mtajibu nini mbele za Mungu siku itakapofika??
Namuomba Mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi wale wote waliouawa bila hatia! |
| 23 | Christina Micah | |
| 24 | janet | Ni kweli inabidi tuachane na imani ptofu kwamba viungo vya wenzetu hawa ni mali. na inabidi serikali ikemea kabisa tabia hii ya kuwaua |
| 25 | kimwaga francis | nina shiriki kupinga mauji ya ndugu zetu wa kitanznia albinos.mimi nipo tayari kutoa kwa hari na mali mchango wangu.zaidi kuhusu kutafuta ulinzi wa ndugu zetu hawa,mimi nimtanzani ninaeishi nchi za nje. |
| 26 | LKU | |
| 27 | Baby | Niingependa serikali ingilie kati katika suala hili kitu ambacho kitasaidia kwa wenzetu maalbino kuendelea kuisha |
| 28 | Anonymous | Niingependa serikali ingilie kati katika suala hili kitu ambacho kitasaidia kwa wenzetu maalbino kuendelea kuisha |
| 29 | Eliabu Thomas | Tuna kila sababu ya kuilazimisha serikali kuchukua hatu maana huu ni uuaji na tena sharti ukomeshwe. Serikali kama imeshindwa basi iombe msaada kutoka nje |
| 30 | Charles Mwafongo | Tatizo la mauja ya albino limekuwa kubwa sasa.Ndugu zetu hawa wanaishi kwa kujifichafichwa kama vile hawastahili kuishi.Ni wajibu wetu sote kama jamii kuwalinda lakini serikali inawajibu mkubwa zaidi.Naiomba serikali iliangalie swala hili kwa mapana na marefu kwani naamini serikali haishindwi kupambana na swala hili. |
| 31 | kanainyemu | NI KITU KIZURI MMEINTRODUCE, MUNGU AKUPENI NGUVU, HAKIKA HILI LINAWEZEKANA |
| 32 | mohamed selemani | naungana na bwana pius kupiga vita zidi ya maalibino nikitendo cha kusikitisha sana kwanchi yetu.nanijambo laabu sana.mudy wa lstamburi uturuky. |
| 33 | Amani | |
| 34 | lily | wen i heard about this i was very disappointed by my fellow tanzanian,why killing another human being bcz of ur stupidity. this is becz people are not educated enough,
na i think hao masangoma wafungiwe wao ndio sababu kuu. |
| 35 | Paul | tusimame pamoja kuzuia uharamia huu |
| 36 | Peter Situmbeko Nalitolela | |
| 37 | Dan K Ngowi | It sad to learn that we (Tz) we always make news with wrong reasons. Its unfortunately to the country and specific to our albinos. We liev in 21st century where human being strive to make impact to the World we are living. Controversy we kill our fellows for unjustifiable reasons. We have to educate our people to create senseful society. |
| 38 | Mango Moses | |
| 39 | anna magege swai | I'M STRONGLY CONDEMING THE KILLING OF ALBINOS. THIS HAS TO STOP, AS A COUNTRY AND AS A NATION, WE HAVE A DUTY TO PROTECT THE MINORITY INDIVIDUALS WHO ARE SUFFERING BECAUSE OF THE COLOUR OF THIER SKIN. |
| 40 | Anonymous | Napingina na mauaji ya Albino. Watu waelimishwe na tumuogope Mungu. |
| 41 | Anonymous | let's stop this cruelty to mankind. |
| 42 | julius | I extremely hate these evil people who kill albino. |
| 43 | Muga Raymond | Ignorance leads people to have negative believes, so i think its the religion institution responsibilities to educate people using the words of the Lord, and that's the only way to stop all these madness. |
| 44 | Maria Sarungi Tsehai | Naomba nianze kwa kutoa pole kwa jamii nzima ya ndugu zetu waalbino! Tuko pamoja na tutaendelea kuwatetea na kupinga vikali uonevu, udhalilishaji, dhuluma na mauaji yanayofanywa dhidi yenu. |
| 45 | Anzamen Mollel | Hawa ni binadamu kama sisi,wana haki zote za kibanadamu,iweje wawindwe kama digi digi porini?ni lazima maiaji haya yapingwe kwa nguvu zote? |
| 46 | Anonymous | |
| 47 | evarist magesa | Natumia nafasi hii kulaani mauaji ya albino,sote ni binadamu na albino ni binadamu,siamini kweli kama viungo vya albino vinaleta utajiri,ingekuwa hivyo basi baadhi ya binadamu wangekata viungo vyao ili wawe matajiri,kwani albino si binadamu. |
| 48 | Renatha Wandelt | Shukurani kwa mwanzishaji wa mjadala huu. Mtu mmoja hawezi kufanya kila kitu ila anaweza kufanya kitu. Naimani kwa kila mmoja wetu kufanya kitu basi tutakamilisha malengo yetu, na hatimaye wenzetu kuwa na amani, kwani hakuna anayependa kuwa hivyo. Mungu atusaidie swala hili litokomee kabisa.
Mungu ibariki Tanzania |
| 49 | NWN | Ningependa kutoa maoni yangu kuhusu kupinga mauaji ya Albinos, kwanza ni jambo la aiubu sana kuona kuna watu wanao abudu uchawi na utajiri bila kujali ubinadamu, kwa kuwauwa ndugu na jamaa zetu kinyama kiasi hicho. Pili tusisahau hao ni binadamu kama sisi, na viongozi wa nchi wahusika inabidi waingilie kati na kutoa adhabu kubwa kwa wote wanao husika, ili kuondoa na kisimamisha mauaji hayo ya kikatili. Tunajivunia nchi yetu ina amani tukiwa nje ya nchi, hii haina tofauti na vita ya ukabila, kisiasa ama dini vinavyoweza kuwafanya watu kukimbia nje ya nchi, hawakuomba kuzaliwa hivyo wakimbilie wapi? na je serikali na wanasheria wake wanachukua hatua gani za kukabiliana na hao wauaji? kwasababu kama wangechukuliwa hatua kali za kisheria hata kama walikuwa wameahidia mamilioni ingebidi wakatae. Kwani wangejua kifungo cha maisha na wao kina wasubiri. Hii ni kukiuka haki za bina damu kwa kuwaondolea uhai wao, kama wakiweza kutoroka na kukimbilia nchi yeyote ya ulaya basi wangelindwa na kupewa haki zao, ama wazungu wakishituka basi ni dili na kuizalilisha nchi yetu, hili ni jambo la aibu sana nchini kwetu kwani jina la Tanzania lina zidi kwenda mbele kwa kila kitu, na hii ni faida na mafanikio kwa sasa na vizazi vijavyo. Swala hili limenigusa sana kama mtanzania anayependa kupigania haki za wanyonge bila kujali, rangi wala kabila popote nilipo duniani. |
| 50 | NWN | Ningependa kutoa maoni yangu kuhusu kupinga mauaji ya Albinos, kwanza ni jambo la aiubu sana kuona kuna watu wanao abudu uchawi na utajiri bila kujali ubinadamu, kwa kuwauwa ndugu na jamaa zetu kinyama kiasi hicho. Pili tusisahau hao ni binadamu kama sisi, na viongozi wa nchi wahusika inabidi waingilie kati na kutoa adhabu kubwa kwa wote wanao husika, ili kuondoa na kisimamisha mauaji hayo ya kikatili. Tunajivunia nchi yetu ina amani tukiwa nje ya nchi, hii haina tofauti na vita ya ukabila, kisiasa ama dini vinavyoweza kuwafanya watu kukimbia nje ya nchi, hawakuomba kuzaliwa hivyo wakimbilie wapi? na je serikali na wanasheria wake wanachukua hatua gani za kukabiliana na hao wauaji? kwasababu kama wangechukuliwa hatua kali za kisheria hata kama walikuwa wameahidia mamilioni ingebidi wakatae. Kwani wangejua kifungo cha maisha na wao kina wasubiri. Hii ni kukiuka haki za bina damu kwa kuwaondolea uhai wao, kama wakiweza kutoroka na kukimbilia nchi yeyote ya ulaya basi wangelindwa na kupewa haki zao, ama wazungu wakishituka basi ni dili na kuizalilisha nchi yetu, hili ni jambo la aibu sana nchini kwetu kwani jina la Tanzania lina zidi kwenda mbele kwa kila kitu, na hii ni faida na mafanikio kwa sasa na vizazi vijavyo. Swala hili limenigusa sana kama mtanzania anayependa kupigania haki za wanyonge bila kujali, rangi wala kabila popote nilipo duniani. |