Powered by iPetitions - start your online petition now

The petition


Ndugu,
Kwa muda mrefu sasa nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na wimbi la mauaji ya ndugu zetu Albinos.Pamoja na kulaaniwa na wanajamii wengi na hatua mbalimbali ambazo serikali imejaribu kuzichukua,wimbi la mauaji limezidi kuenea.Hivi leo,wenzetu hawana amani tena ndani ya nchi.Maisha yao yanatishiwa kila kukicha.

Wimbi hili limezidi kuipaka nchi yetu matope.Kama wanajamii,hatuwezi kukaa kimya.Ni wazi kwamba juhudi za ziada zinahitajika kutoka serikalini ili kukomesha mauaji hayo ambayo msingi wake ni imani potofu kwamba viungo au sehemu mbalimbali za mwili wa albino ni njia mojawapo ya kujipatia utajiri.

Ni kwa kuzingatia hilo unaombwa kushiriki katika kupinga,kulaani na kuishinikiza serikali iongeze juhudi za kupambana na janga hili ambalo limeshakuwa la kitaifa.Unachotakiwa ni kutia sahihi.Zikitimia sahihi 100,000,zitapelekwa kwa Waziri mhusika kufikisha ujumbe kwamba juhudi za ziada zinahitajika.Tafadhali shiriki.Asante

Sign the petition

Fields marked  *  are required.

* Name:
* Email:
Comments:
Display my name as anonymous on the signatures list
Yes, I want iPetitions to contact me on similar campaigns or petitions.
  
 

 

Petition sponsor

 

Links



 

The views expressed in this petition are solely those of the petition's sponsor and do not in any way reflect the views of iPetitions. iPetitions is solely a provider of technical services to the petition sponsor and cannot be held liable for any damages or injury or other harm arising from this petition. In the event no adequate sponsor is named, iPetitions will consider the individual account holder with which the petition was created as the lawful sponsor.