Balozi Daraja Ajiuzulu!

Balozi zetu nyingi zinalalamikiwa kwa kutowajali Watanzania na kutoa huduma duni za kibalozi na ushirikiano kwa Watanzania katika nchi zilizopo. Ubalozi ambao bila ya shaka unaongoza malalamiko hayo ni ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ambapo mkuu wake ni Balozi Andrew M. Daraja. Kwa kuzingatia ukweli kuwa Balozi Daraja ameshindwa vibaya katika mambo kadhaa ambayo yanaanishwa hapa: http://www.mwanakijiji.podomatic.com. Miongoni mwa hayo: a. Kushindwa kutekeleza diplomasia ya Kiuchumi kama ilivyoelekezwa na Wizara ya Mambo ya nje kwa kutumia makabrasha mbalimbali na semina ya mabalozi ya Bagamaoyo. b. Ameshindwa kujenga mahusiano na Watanzania waishio Marekani na hivyo kutowatumia ipasavyo katika kutekeleza diplomasia ya kiuchumi na hivyo kusababisha Watanzania kutokuwa na imani na balozi huyo. c. Ameshindwa kutumia nafasi iliyopo ya uhusiano mzuri kati ya Marekani na Tanzania kunufaisha Tanzania kwa kuvutia watalii wengi zaidi na wawekezaji wengi zaidi na biashara ya Marekani kwa kutumia AGOA, mkataba wa Anga huru. Hivyo basi sisi Watanzania tunatoa mwito wa kumtaka Balozi Daraja ajiuzulu au Rais aamua kumwondoa katika wadhifa huo muhimu ili kutoendelea kupoteza muda mwingi.

Sponsor

Mwito huu unadhaminiwa na KLH News, Taasisi ya Kitanzania ya Demokrasia, Maendeleo na Amani, Baraza la Gumzo, na Uwanja wa Mapambazuko. Wadhamini wengine ni jambophotos.com na jamboforums.com

Links

http://www.mwanakijiji.podomatic.com http://www.blog.co.tz/mapambazuko http://www.phpbbcity.com/forum/baraza.html http://www.jamboforums.com http://www.jambophotos.com http://www.bongoradio.com

Discussion

No comments yet.

join the discussion

Recent signatures

 • username

  Kweyamba, Tanzania, United Republic of

  7 years ago Comments: Balozi anapimwa utendaji na aliyempa kazi. Hivyo mwachie hiyo kazi.
 • username

  DENIS, Uganda

  7 years ago Comments: AONDOLEWE KABISA KAMA ANASHINDWA KUWATHAMINI NYIE MLIOKO UKO,,KAMA ANAWAONA WAKIMBIZI AWATAFUTIE BASI REFUGEE CAMP..WATU KAMA HAWA HAWAITAJIKI MIDA KAMA HII EE MOLA MUONDOE KABLA AJAJIUZULU MAAN NDIO STYLE WANAYOANZA KUTOKA NAYO SIKUHIZI
 • username

  Mkandara, United States

  8 years ago Comments: Ameshindwa kuiongoza wizara
See more

Petition highlights

There are no highlights yet.